In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player


Utamu wa Shule, Ladha ya Degree.
Vyuoni Tanzania Blog is an open discussion blog. This blog is NOT owned, affiliated or operated by Tanzania Commission For Universities.

Itangaze Blog Hii Kupitia

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon

Tuesday, April 12, 2011

PROF. MAYUNGA H.H. NKUNYA AAGWA RASMI..


Baada ya kufanya kazi kama katibu Mtendaji kwa miaka mitatu, hatimaye Prof. Mayunga Nkunya ameagwa rasmi kwenye sherehe iliyofanyikia katika ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza. 
 Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa Waziri wa Elimu na Mafuzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa.

 Prof. Mayunga H.H Nyunya
Muagwa Prof. Mayunga Nkuya akiwashukuru kwanza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa umoja wa wakuu wa vyuo Vikuu (CVCPT) Prof. Idris Mshoro na Wafanyakazi wa Tume ya Vyuo vikuu (TCU) kwa ushirikiano wao ambao bila kuwepo hayo TCU isingepiga hatua kubwa hivyo kimaendeleo.
Prof. Nkunya amemaliza muda wake TCU na sasa anaenda kuwa katibu mtendaji wa Baraza la Umoja wa Vyuo Vikuu vya Jumuiya ya Africa Mashariki (IUCEA) ambayo makao yake makuu yako Kampala Uganda.



 Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Prof. Awadhi Mawenya alikuwepo nae akatoa nasaha zake kama Baba na Mlezi wa Tume

 Mwenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa vyuo vikuu hapa Nchini Prof. Idris Mshoro alipata nafasi ya kuwawakilisha makamu wakuu wenzake kwa nasaha na shukrani


 Hapa ni wakati sherehe zikiendelea Mgeni rasmi anaonekana kuvutiwa na MC (hayupo Pichani)


 Ukafika wakati wa kumzawadia muagwa ambaye alikuwa na Mke wake mama Nkunya. Mgeni Rasmi Dr. Shukuru Kawambwa anamkabidhi Prof. Nkuya zawadi iliyoandaliwa na wafanyakazi wa TCU


 Ikawa ni pamoja na pongezi na mikono ya kutakiana kila la kheri kwa kazi na mwanzo wa kuanza majukumu mapya huko IUCEA- Kampala Uganda


 Ukafika wakati wa Mnuso, Wafanyakazi na wgeni waalikwa walijichotea kinamna hii...


 Prof. Njozi wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Muslimu University ya Morogoro (MUM) akibadilishana mawazo na Prof. Yunus Mgaya aliyemwakilisha Makamu mkuu wa chuo cha Dar es Salaam (UDSM)


Baada ya hapo wadau wakajimwaga kusakata sebene kama hivi; Mama Nkuya akijimwaya na baadhi ya wafanyakazi wa tume.

Posted by Mwanachuotz

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru