In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player


Utamu wa Shule, Ladha ya Degree.
Vyuoni Tanzania Blog is an open discussion blog. This blog is NOT owned, affiliated or operated by Tanzania Commission For Universities.

Itangaze Blog Hii Kupitia

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon

Wednesday, April 6, 2011

SCHOLASHIPS FOR WOMEN ENTREPRENEURS

BUSINESS SCHOOL  OFFICE OF THE DEAN


University of Dar es Salaam Business School (UDBS) ikishirikiana na Columbia Business School ya Marekani, kwa mara ya pili, inawapa fursa ya pekee wanawake wajasiliamali kwa kuwapatia ufadhili kutokaThe Goldman Sachs Foundation ya Marekani kwa ajili ya kusoma kozi ya “Advanced Certificate in Entrepreneurship and Business Management” Kozi inatolewa kwa mwaka mmoja nani wakati wa jioni tu. 
Lengo kuu la kozi hii ni kuwawezesha wajasiliamali kuendesha na kukuza biashara zao kitaalamu zaidi na kwa faida. Kwa kupitia wahadhiri waliobobea katika masomo ya biashara kutoka katika vyuo hivi viwili washiriki wataweza kuongeza uwezo wa kutambua na kunufaika na fursa mbalimbali za kibiashara, watakuza uwezo wa uendeshaji wa biashara, wataweza kuandaa michanganuo ya biashara yao inayokubalika katika taasisi za mikopo na wataunganishwa na vyanzo mbalimbali vya mitaji. 

Mwombaji wa ufadhili anatakiwa awe mwanamke mjasiliamali mwenye biashara na awe na uwezo wa kuongea na kuandika lugha ya kiingereza kwa ufasaha. 

Kozi itaanza Terehe 6. 7. 2011 na kumalizika mwezi June mwaka 2012. Mwisho wa kupokea fomu za maombi ni tarehe 13.5.2011.  Fomu za maombi zinapatikana kwa Dean, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, jengo la UDBS, chumba namba 310, au katika tovuti ya www.udbs.udsm.ac.tz .

Kwa maelezo zaidi piga simu namba:
  0715-004-280 au 0767-004-280 

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru