In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player


Utamu wa Shule, Ladha ya Degree.
Vyuoni Tanzania Blog is an open discussion blog. This blog is NOT owned, affiliated or operated by Tanzania Commission For Universities.

Itangaze Blog Hii Kupitia

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon

Tuesday, April 12, 2011

TCU: UDAHILI VYUO VIKUU KWA MWAKA WA MASOMO 2011/2012 UMEANZA

Mwombaji anapaswa ajidahili kwa kutumia Simu ya mkononi yenye kutumia mtandao wa Vodacom tuu kwani mitandao mingine haina mkataba na TCU

 Baada ya hapo mwombaji anunue vocha ya malipo, Zinapatikana CRDB Bank matawi yote nchi nzima kasoro tawi la Mlimani City, PPF na Kariakoo.

Kisha awe anafahamu namba zake za mitihani ya kidacho cha Nne na cha Sita
angalizo Muhimu ni kuwa mwombaji akishafanikiwa kijidahili asibadili namba yake ya simu au anwani yake ya barua pepe kwani mawasiliano yeyote na TCU yatakurudia kupitia anwani hizo ambao zitakuwa zimehifadhiwa kama kumbukumbu muhimu za waombaji.

Muhitimu akiperuzi kwenye mtandao kw maandalizi ya kujidahili Chuo kinanukia

Tunapenda kuwatangazia Wanaopenda Kujiunga na Vyuo Vikuu au Taasisi za Elimu ya Juu Hapa Nchini Kuwa Tumefungua Mfumo wa Pamoja wa Udahili “Central Admission System” Kwa mwaka wa Masomo 2011/2012

·        Wenye sifa Kujidahili na mfumo ni waliomaliza kidato cha Sita tangu mwaka 1988 na kuendelea

·        Waombaji Waliomaliza kidacho cha Sita Mwaka Huu 2011 Wataanza kujidahili punde tuu maokeo yao yatakapotoka.
·        Waombaji Waliomaliza Vidato Vya  Sita nchi tofauti na Tanzania wataanza kujidahili kuanzia tarehe 30 Aprili Mwaka huu 2011 ambapo watapaswa kulipia shilling Elfu Sitini (60,000) kupitia TCU CAS Acc. No. 01J1026795702) the swift code: CORU TZ Branch code: 3314

·        Waombaji wanapaswa wajidahili kupitia Internet kwenye tovuti ya Tume ya Vyuo Vikuu http://www.tcu.go.tz/ au kwa simu za kiganjani ambazo nizatumia mtandao wa vodacom tuu, Mitandao mingine haihusiki.
·        Waombaji wa ndani wanapaswa walipie Shilingi Elfu Thelathini tuu (30,000) kwa njia ya Vocha zinazopatikana kwenye matawi ya CRDB Bank nchi nzima kasoro matawi ya Mlimani City, Kariakoo na PPF Tower yaliyopo Dar es Salaa.

·        Maelezo ya Namna ya kujisajili kwa njia Zote Mbili (Internet na SMS) yanapatikana kwenye kitabu cha Mwongozo wa mwombaji kinachopatikana kwenye Mtandao wa TCU au kwenye Maktaba za mikoa yote na haviuzwi.

·        Mwombaji akifanikiwa kujidahili anapaswa atunze Kumbukumbu zake Bila kuzisahau au kumpa mtu mwingine, hii ni Pamoja na kutunza namba ya simu au barua Pepe aliyotumia kujidahili  Ikiwa ni pamoja na Jina la utumaji “User name”

Imetolewa na Katibu Mtendaji
Tume ya vyuo Vikuu (TCU), Dar es Salaam

BLOG Hii ITAWEKA MTIRIRIKO WOOTE WA NAMNA YA KUJIDAHILI HIVI PUNDE Endela kutufatilia

By Mwanachuotz

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru