In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player


Utamu wa Shule, Ladha ya Degree.
Vyuoni Tanzania Blog is an open discussion blog. This blog is NOT owned, affiliated or operated by Tanzania Commission For Universities.

Itangaze Blog Hii Kupitia

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon

Wednesday, April 6, 2011

YA PPF NI WIZI NA SI VINGINEVYO...

Mwonekano wa Jengo la PPF Makao Makuu

Jana tumeanza kuangalia suala la malipo ya zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa wakurugenzi sita ndani ya shirika la Pensheni la Mashirika ya Umma (PPF). Tuliona baadhi tu ya invoices za malipo kwa Wakurugenzi hao. Malipo hayo toka mwanzo yalizua mgogoro ndani ya PPF baada ya aliyekuwa Mhasibu Mkuu kutotaka kulipa na kujikuta akigongana na viongozi wake wa juu (ambao walikuwa walengwa wa malipo hayo). Pamoja na nia yake njema ya kujaribu kuliokolea shirika fedha hizo na kujaribu kusimamia utawala bora Mhasibu huyo aliondolewa makao makuu na baada ya kumrusha huko na huko amejikuta akirushwa Mbeya ambako juhudi za mwisho sasa hivi zinataka kuhakikisha anatolewa kabisa kwenye Shirika. Jitihada zake hazijapata mtetezi ndani ya serikali. Kukosekana kwa sheria ya kuwalinda Whistleblowers ni kizuizi kikubwa kwa watu kama hawa kujitokeza hadharani kwani ndio wanapata makali ya hasira ya viongozi wanaoumbuliwa.

Kutokana na mgongano uliotokea baada ya malipo kufanyika Shirika ikabidi liitishe Kikao cha ndani na ajenda ikiwa ni kujadili ripoti ya Wakaguzi wa Nje waliotumwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Barua hii sehemu kubwa inaelezea kile ambacho wakaguzi hao walikipata na mapendekezo yao.

Wakaguzi wa nje (External Auditors) wa TAC Associate wanaofanya Audit kwa niaba ya Controller and Auditor General (CAG) wameeleza kuwa malipo hayakuwa sahihi. Walipeleka ukaguzi wao kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Gray Mgonja ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi PPF ambaye hakuufanyia kazi - labda kutokana na matatizo yake mwenyewe. Pia walipeleka nakala kwa CAG. Angalia ukurasa wa nane wa nakara ya ripoti ya TAC
Ukipitia ripoti ya Mkaguzi Mkuu ya 2007/2008 (kipindi cha Malipo haya) huwezi kuona yale ambayo yanatajwa katika maoni ya wakaguzi hawa ambayo kama yangepewa uzito unaostahili leo hii (baada ya malipo mengine kufanyika kama inavyotarajiwa) tusingekuwa tunayazungumzia. Ripoti Kamili Inakuja siku chache zijazo - Kurasa karibu 50 ambazo zitashtua watawala wetu. Tukitoka hapa tunaenda kule kwingine ili tusije kuonekana tunaing'ang'ania PPF!
Kundi hilo lililolipwa kiasi hicho ni hawa wafuatao na kiasi cha fedha ambazo walijilipa kama sehemu ya “mafao” yao kwa mwaka 2008.

1. Baduru Msangi -Mkurugenzi wa Pensions Tshs. 220,000,000 (Milioni 220)
2.Hossea Kashimba -Chief Internal auditor Tshs. 220,000,000 (Milioni 220)
3. Michael Mjinja- Director of Commercial Services-Tshs 172, 000,000(Milioni 172)
4. Charles Chenza-Director of Investiments- Tshs 172, 000,000 (Milioni 172)
5. Martin Mmari Director of Finance Tshs. 172,000,000 (Milioni 172)
6. Carina Wangwe-Director of computer Services. Tshs. 130,000,000 (Milioni 130)

Mwaka 2010 Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Erio alilipwa shilingi 520,000,000 yaani shilingi Milioni 520! Hii ni sasa na nusu bilioni!

Kwa kadiri ya kwamba Serikali itaendelea kukaa kimya bila kuonesha kuchukua hatua tutaendelea kufunua sakata hili kwa kuendelea kuweka hadharani nyaraka mbalimbali zinazohusiana na utendaji mbovu katika mashirika haya ya hifadhi ya jamii... Hatua zozote za kuchunguza PPF ni muhimu kuhusisha mifuko yote mingine. Natumaini Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma itakuwa na la kusema japo sijui kwanini itakuwa hivyo sasa kwani jambo hili lina miaka mitatu sasa na hasa tukizingatia kuwa malipo mengine yatakuwa yamefanyika jana na mengine kufanyika leo huku mmoja wa waliolipwa safari iliyopita atadai kulipwa tena as "end of employment" kwani anakwenda Bodi mpya kusimamia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

By M M Mwanakijiji 
 Vyanzo vya habari hii ni hivyo hapo chini
Tz Job Vacancies www.kazibongo.blogspot.com
International NGO Jobs www.worldngojobs.blogspot.com

To unsubscribe from this group, send email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru